Kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesisitiza kuwa bado anaungwa mkono kikamilifu na uongozi wa klabu pamoja na mashabiki, licha ya matokeo mabaya yaliyoitikisa timu hivi karibuni. Liverpool wamepoteza mechi tatu mfululizo, ikiwemo kichapo cha 2-0 kutoka kwa PSG kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Shinikizo limeongezeka kwa kocha huyo wa Kiholanzi kufuatia matokeo hayo mabaya, pamoja na kupigwa 4-0 na Manchester City kwenye FA Cup na kupoteza mechi ya ligi dhidi ya Brighton. Hata hivyo, Slot anaamini bado ana imani ya viongozi wakuu wa klabu, akiwemo mkurugenzi wa michezo Richard Hughes na CEO Michael Edwards.
Kocha huyo pia ameguswa na namna mashabiki walivyoendelea kuwaunga mkono hata katika nyakati ngumu. Akiwa Paris, alisema mashabiki waliendelea kuimba na kuwapa moyo licha ya timu kuonesha kiwango cha chini uwanjani, jambo ambalo limempa nguvu ya kuendelea kupambana.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Pamoja na hali hiyo, kuna changamoto nyingine nje ya uwanja, ambapo mashabiki wanapanga maandamano kupinga ongezeko la bei za tiketi. Slot ametambua hali hiyo lakini amewaomba waendelee kuipa timu sapoti, hasa katika mechi za nyumbani ambapo nguvu ya mashabiki imekuwa silaha muhimu.

Kwa sasa, Liverpool wanahitaji kurejea haraka kwenye kiwango chao ili kuokoa msimu wao. Imani ya uongozi na mashabiki inaweza kuwa nguzo muhimu kwa Slot katika kipindi hiki kigumu cha mabadiliko.

