Hakika ulikuwa ni usiku wa kihistoria uliofunikwa na ufundi wa kila aina ambao kwa hakika umeleta tafsiri halisi ya usiku wa mabingwa Ulaya. Ni mechi ambayo kwa hakika tunaweza kusema ni bora zaidi ya mechi nyingine zilizopita kwenye michuano hii ya klabu bingwa kutokana na historia iliyotengenezwa.
Ni mechi ambayo wengi husema mtoto hatumwi dukani ikiwa na maana kwamba ukitoka dakika kadhaa kule kurudi tu unakutana na mambo tofauti. Ndicho kilichokuwepo jana ndani ya dakika kumi za mchezo tayari kulikuwa na magoli yasiyopungua manne. Hakika ilikuwa ni mechi ambayo haipimwi kwa namna yoyote ile.
Walikuwa ni wenyeji Manchester waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Sterling ambaye alipiga mkwaju uliomshinda mlinda mlango Lloris ambaye kwa hakika alionekana ni nguzo imara ndani ya kikosi hicho baada ya kuondoa hatari nyingi mbele ya City walioonekana kuwa na hasira sana kwenye mechi hiyo.
Haikuchukua hata dakika tano Son ambaye amewatesa sana City kwenye michuano hii akaweka kamba nyingine na kuwafanya City kurudi tena kwenye deni lao la kuhitaji magoli mawili zaidi ili kupenya kwenye hatua inayofuata ya michuano hiyo. Ubora wa City haukuonekana mbele ya safu ya ulinzi ya Spurs ambao walionekana kuwa makini mno.
Magoli hayo ya Son hayakuweza kudumu sana kwa kipindi hicho kutokana na makosa yaliyofanywa na safu ya ulinzi kidogo na kuwaruhusu City kupata goli la kusawazisha makosa yao. Utamu wa mechi hiyo ulichagizwa na pasi nyingi zilizochezwa na timu zote mbili kwa kuleta maana nzuri ya soka la wakubwa.
Hakuna asiyewajua Spurs, ni timu inayocheza mpira mwingi kwa maana kwamba wana uwezo wa kumiliki mpira, kuuchezea wanavyotaka na kasi kubwa wanapokuwa na mpira. Jambo hilo limekuwa likiwasumbua wakubwa wengi wanaokutana naye kwa sababu ana kila mbinu ya kuhakikisha anachukua matokeo kwenye mechi yake. Hata wangekutana na Barcelona kwa hakika hakuna maajabu anbayo yangetokea kutokana na uchezaji wao na ubora walionao.
Baada ya ushindi huo sasa ambao wameupata kutokana na faida ya goli la nyumbani na kufanya matokeo kuwa 4-4 basi yanampa nafasi moja kwa moja kuandika historia yake ya kuweza kufuzu katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza tangu wawe chini ya Pochettino huku wakiwa hawajafanya usajili wa aina yoyote ile. Wameanza vizuri ndani ya uwanja wao wa nyumbani kwa kushinda mechi zao walizozicheza pale.
Safari yao hiyo itawakutanisha na Ajax ambao wamekuwa na safari ngumu sana hadi kufikia hapo kutokana na uzoefu na aina ya timu alizokutana nazo ndani ya hatua hiyo. Kwa hakika wawili hawa wanaenda kukutana wakiwa wameonesha ukomavu wao mkubwa kwenye michuano hiyo pamoja na ugeni walionao. Kinachosubiriwa kwa sasa ni kujua tu nani anaanzia wapi na anamalizia wapi.


Issa
Ni noma