Ten Hag Anaamini Wachezaji Wake Watafanya Vizuri Mechi Ya Jumapili.

Kocha mkuu wa Manchester United Erik ten Hag anatumaini kuwa wachezaji wake wametunza mabao kwaajili ya mechi ijayo, baada ya kuonyesha matokeo mabaya katika ushindi wao wa 1-0 wa Ligi ya Uropa dhidi ya Omonia Nicosia siku ya jana.

 

Ten Hag Anaamini Wachezaji Wake Watafanya Vizuri Mechi Ya Jumapili.

Bao la ushindi la Manchester United lilifungwa na Scott McTominay katika dakika ya 90 ya mchezo kumalizika kwa 1-0  na kuwa mchezaji wa kwanza wa akiba kufunga bao la ushindi baada ya dakika ya 90 katika mechi ya Uropa kwa Mashetani Wekundu tangu Ole Gunnar Solskjaer alipofunga bao la kipekee kwenye Ligi ya Mabingwa 1999.

Alipoulizwa kama ushindi ndio jambo kuu, Ten Hag aliiambia BT Sport: “Hapana, sivyo, kwa sababu mpira wa miguu ni kufunga mabao.  “Tulitengeneza nafasi nyingi sana lakini tulipiga wavuni mara moja tu, timu ni mvumilivu,

 

Ten Hag Anaamini Wachezaji Wake Watafanya Vizuri Mechi Ya Jumapili.

Ten Hag aliendelea kusema kuwa hana wasiwasi kwasababu katika kila mchezo wanafunga na wana imani kuwa wanaendelea na hilo na wanatumaini wanatunza mabao yao kwaajili ya wikiendi.

Kocha huyo alisema kuwa wakati wa mapumziko walihitaji kuweka umakini na unapocheza dhidi ya mpinzani mwenye uwezo mkubwa wa kujilinda na usifunge bao unakuwa na papara, pia unaweza kuzembea na kupoteza mpira kisha wakavunjika.

“Tulijua tunahitaji ushindi usiku wa leo lakini wangetimuliwa pia,” alisema. “Neil Lennon ni kocha mzuri na hakuna michezo kama hii ambayo huwa rahisi. Kila mtu amefurahishwa na matokeo.

Ten Hag Anaamini Wachezaji Wake Watafanya Vizuri Mechi Ya Jumapili.

Manchester United mpaka sasa wapo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi nne ushindi mara tatu na kupoteza mechi moja, pointi 9 huku kinara akiwa ni Real Sociedad akiwa na pointi 12 na lengo lao ni kushinda kundi hilo.

Siku ya Jumapili United atamkaribisha Newcastle United Old Trafford kwenye mchezo wa Primia Ligi ambapo mechi hiyo ikionekana kuwa sio rahisi kwa mashetani hao baada ya Newcastle kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo.

Ten Hag Anaamini Wachezaji Wake Watafanya Vizuri Mechi Ya Jumapili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.