Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amethibitisha kua wapo kwenye mazungumzo ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu ambao mikataba yao ipo ukingoni.
Kocha huyo amezungumza mapema leo kua klabu hiyi imeanza rasmi mazungumzo na wachezaji wake muhimu ili kuwaongezea mikataba ya muda mrefu ili waendelee kusalia klabuni hapo, Kuna wachezaji kadhaa ambao mikataba yao inakaribia kumalizika na kocha huyo anawahitaji kwenye mradi wake wa kujenga timu hiyo.
Wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni ni Marcus Rashford, Diogo Dalot, Luke Shaw, Fred na kocha Ten Hag ameweka wazi anataka kutengeneza timu ya muda mrefu na wachezaji hao wanatakiwa kua ndani ya timu hiyo hivo wanahitajika kuongezewa mikataba.
Siku za hivi karibuni klabu ya Manchester United kupitia kocha wake ilielezzwa wapo kwenye mkakati wa kuwaongezea wachezaji wake mikataba ambao mikataba yao inaelekea ukingoni na wachezaji waliotajwa sana ni Marcus Rashford pamoja na Diogo Dalot, Lakini kocha huyo leo amezungumza na kuweka bayana sio hao tu akiwaongeza Fred na Luke Shaw.
Manchester United chini ya Erik Ten Hag inataka kutengeneza timu bora na ya muda mrefu, Hivo viongozi hawana budi kusikiliza mahitaji ya mwalimu kwajili ya ustawi wa timu hiyo ambayo inataka kurejesha makali yake yaliyopotea kwa muda mrefu.

