Inaonekana Erik Ten Hag hanamuda wa kupoteza, ameianza kazi ya Manchester United kimkakati zaidi. Matokeo yake ni?

Ten Hag amebakiza michezo 2 tu ya kuiongoza Ajax kabla hajaachana rasmi na klabu hiyo na kutua Manchester Airport kwa kazi ya miaka 4 kule Old Trafford. Pamoja na hilo, ameshatwaa ubingwa wa Ligi ya Uholanzi na, hana presha yoyote na michezo iliyobaki.

Mikakati ya kuisuka United mpya imeanza, John Murtough ameendelea kufanya usafi kwenye safu ya uongozi wa klabu hiyo na pengine panga pangua zikaendelea kwa siku za usoni.

Ten Hag, Ten Hag Kazi Imeanza United, Meridianbet
Erik akizungumza jambo na Mitchell.

Inaripotiwa kuwa, muda mfupi baada ya kutwaa ubingwa wa Uholanzi, Erik ameongoza kikao kazi kilichohudhuriwa na Mkurugenzi wa Soka wa United, John Murtough pamoja na Mitchell Van Der Gaag anayetajwa kufikia makubaliano ya kuungana na Erik Ten Hag kule Old Trafford kama kocha msaidizi.

Za chini ya kapeti zinasema, miongoni mwa ajenda za kikao hicho ni mipango ya kimkakati kuelekea dirisha la usajili mwezi ujao ambapo, baadhi ya wachezaji wataondoka United na kupisha nafasi ya wachezaji wengine kusajiliwa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa