Tetesi zinasema, Bayern Munich wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua mchezaji wa United Paul Pogba, 29 huku Juventus, Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City wakiwa tayari kuwinda saini ya kiungo huyo.

Newcastle itawasilisha ombi la kumsajili katika msimu wa joto mshambuliaji wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25, kama lengo la kipaumbele chake.

Tetesi zinasema, Chelsea wanataka kukamilisha usajili wa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, mapema katika dirisha la kiangazi.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Meneja Pep Guardiola atafikiria kuongeza mkataba wake na Manchester City, ambao unamalizika 2023, msimu huu wa joto.

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 27, anatarajia kujiunga na moja ya klabu maarufu barani Ulaya iwapo ataondoka Etihad msimu wa joto.

West Ham haitafanya mazungumzo zaidi na kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice hadi dirisha la usajili la majira ya kiangazi litakapofungwa baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kukataa kandarasi ya miaka minane yenye thamani ya £83m.

Tetesi zinasema, Aston Villa wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Leeds na England Kalvin Phillips, 26.

Tetesi zinasema, endapo Barcelona watampoteza De Jong msimu wa joto, meneja Xavi anamtaka kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 27.

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 28, anataka kusalia Chelsea msimu huu wa joto licha ya kuwa na wakati mgumu Stamford Bridge tangu alipojiunga akitokea Inter Milan msimu uliopita wa joto.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Beki wa Liverpool na England Joe Gomez, 24, anasakwa na meneja wa Aston Villa Steven Gerrard msimu huu wa joto.

Winga wa Arsenal Reiss Nelson, 22, atafanya mazungumzo na Mikel Arteta kuhusu hatma yake baada ya mkopo wa mwaka mzima huko Feyenoord.

West Ham wanataka kumsajili mshamuliaji wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard, 29, ambaye alitumia msimu mmoja kwa mkopo na The Hammers wakati mkataba wake utakapomalizika msimu huu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa