Ten Hag Kocha Bora Mwezi Febuari Epl

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amefanikiwa kua kocha bora wa ligi kuu ya Uingereza mwezi Febuari baada ya kuiongoza timu hiyo kupata matokeo mazuri ndani ya mwezi huo.

Ten Hag amefanikiwa kubeba tuzo hiyo baada ya kuwashinda makocha wenzake kama Antonio Conte wa Tottenham Hotspurs, Marco Silva wa Fulham, Hiyo ni baada ya kufanikiwa kuiongoza klabu hiyo kwa kiwango kikubwa ndani ya mwezi Febuari.Ten HagKlabu ya Manchester United ndani ya mwezi Febuari imefanikiwa kucheza michezo minne na kufanikiwa kushinda michezo mitatu kati yake, Huku ikisuluhu mchezo mmoja na kujikusanyia jumla ya alama 10 katika michezo minne ni wazi kocha huyo Ten Hag amekua kwenye kiwango bora ndani ya timu hiyo.

Kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi amefanikiwa kushinda tuzo hiyo ikiwa ni mara yake ya pili msimu huu kutwaa tuzo hiyo akifanikiwa kutwaa tuzo hiyo mwezi Septemba mwaka jana, Hivo kuendelea kuonesha ubora wake baada ya kutoa tuzo hiyo mwezi huu.ten hagKocha Erik Ten Hag amekua na wakati mzuri tangu ajiunge na klabu ya Manchester United mapema mwezi Mei mwaka jana, Mpaka sasa akifanikiwa kuipa United taji la kwanza baada ya miaka saba vilevile wakiwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania mataji mengine matatu yaliyobakia baada ya kubeba Carabao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.