Ten Hag: Lindelof Haguswi

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua beki wake raia wa kimataifa wa Sweeden Victor Lindelof haguswi na yupo kwenye mipango yake ya muda mrefu ndani ya timu hiyo.

Kocha Ten Hag yupo tayari kumuachia beki wake raia wa kimataifa wa Uingereza Harry Maguire lakini sio Victor Lindelof ambaye amekua kwenye kiwango bora hasa katika michezo ya mwishoni kitu kilichomfanya kocha Ten Hag kumuamini na kuhitaji kuendelea kua nae kikosini.Ten HagVilabu kama Inter Milan na Frankfurk zililulizia huduma ya beki huyo wa kimataifa wa Sweeden katika dirisha dogo la mwezi Januari, Lakini Man United hawakua tayari kumuachia beki huyo na vilabu hivo vimerudi tena dirisha hilo lakini kocha wa klabu hiyo hayuko tayari kumuachia.

Kocha Ten Hag yuko kwenye mpango wa kuitengeneza timu hiyo kwa muda mrefu na kuirudisha kwenye mafanikio kama ambavyo imekua iifanya kwa miaka kadhaa nyuma, Hivo anahitaji kubakiza wachezaji wake muhimu kwenye kikosi na moja ya wachezaji hao ni Victor Lindelof.Ten HagMwanzoni mwa msimu ilionekana kama Victor Lindelof hatakua na muda mrefu ndani ya timu hiyo kutokana na ufinyu wa nafasi ambao alikua anaupata, Lakini imekua tofauti kwani kocha Ten Hag alimuamini beki huyo kwa kumpa nafasi na Lindelof amelipa fadhila kwa kuonesha kiwango bora.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.