Tetesi zinasema, Lyon wanataka kumnunua tena mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 31, kwa uhamisho huru – miaka mitano baada ya kumuuza kwenda Arsenal kwa £46.5m.
Tetesi zinasema, Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye ataondoka Leicester City msimu huu wa joto.
Tetesi zinasema, Manchester United watapewa fursa ya kumsajili winga wa Real Madrid Mhispania Marco Asensio, 26.
Mshambuliaji wa Manchester City Mbrazil Gabriel Jesus, 25 na mlinzi wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, na kiungo Raheem Sterling, 27 wote wanaweza kuondoka msimu huu wa joto.
Tetesi zinasema, Beki wa Uholanzi Nathan Ake, 27, pia ameambiwa anaweza kuondoka Manchester City na hilo linaweza kufungua njia ya kuhamia Newcastle.
Tetesi zinasema, Beki Mholanzi Sven Botman, 22, anataka kuondoka Lille msimu huu wa joto na anasema AC Milan na Newcastle wana nia ya kumsajili.
Tottenham wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa West Ham kutoka Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, huku mazungumzo kuhusu kandarasi mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yakiwa yamekwama.
Roma wanamnyatia kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 29, mkataba wake na Manchester United utakapokamilika msimu huu, lakini West Ham na Everton miongoni mwa wanaomuwinda kiungo huyo.
Tetesi zinasema, Leeds United wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kulia wa Red Bull Salzburg na Denmark Rasmus Kristensen, 24.
Forest, Norwich City na Huddersfield Town wanapanga mipango ya kumsajili beki wa kushoto wa Angers raia wa Cameroon Enzo Ebosse, 23.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!