Thiago Silva: Naweza Kurejea Milan Kama Kocha

Beki wa kati wa klabu ya Chelsea Thiago Silva amesema kuwa  hadithi yake na Milan tayari imekamilika na amependekeza kuwa anaweza kurejea katika klabu yake ya zamani kama kocha.

 

Thiago Silva: Naweza Kurejea Milan Kama Kocha

Bingwa huyo mtetezi wa  Serie A msimu uliopita atakuwa nyumbani SanSiro kucheza mchezo wa marudiano katika michuano ya klabu bingwa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza akiwa Stamford Bridge kwa mabao 3-0 huku Thiago Silva akiwa ndani ya kikosi hicho kilichoiua Milan.

Hapo awali Silva alitumia misimu mitatu kati ya 2009 na 2012 akiwa na Rossoneri, akishinda Scudetto, kabla ya kuhamia Paris Saint-Germain, ambapo alijiimarisha kama mmoja wa walinzi bora wa kati wa kandanda Ulaya.

Ukubwa wa Ligi ya Mabingwa tangu kuhamia Chelsea umethibitisha kuhama kwa mkongwe huyo kutoka PSG, na Silva sasa amefichua kuwa alikosa nafasi ya kurejea Milan kabla ya kwenda Stamford Bridge. Thiago alisema;

Thiago Silva: Naweza Kurejea Milan Kama Kocha

“Njia yangu Milan tayari imekamilika,” alisema. “Hadithi yangu tayari imeandikwa. Fursa ya kuja hapa ilikuja kabla sijajiunga na Chelsea, lakini haikufanyika.”

Pamoja na hayo, Silva alikiri kuwa anaweza kurejea mara baada ya kustaafu na kuongeza kuwa hadhani kuwa kama anaweza kurudi Milan kama mchezaji katika siku zijazo lakini labda kama kocha.

“Nina furaha sana, nimefurahi sana kurejea SanSiro. Kila kitu ambacho nimepitia na klabu hii kubwa, kinanijia akilini. Wakati wa mchezo itakuwa hivyo zaidi.”

Thiago Silva: Naweza Kurejea Milan Kama Kocha

Acha ujumbe