Tottenham Yaendelea Kuwapa Vijana Mikataba Mipya

Klabu ya Tottenham wanaonekana wana mradi wao wa muda mrefu kwani wamekua wakiwasainisha mikataba mipya na mirefu wachezaji vijana klabuni hapo ambapo alianza Destiny Udogie na leo wamemuongezea mkataba Pape Matar Sarr.

Pape Matar Sarr raia wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 23 ameongezewa mkataba ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2030, Hii inaendelea kuonesha kua klabu ya Tottenham ina mpango wa muda mrefu.TottenhamKijana Pape Matar Sarr amekua kwenye kiwango kizuri msimu chini ya kocha Ange Postecoglou na kua moja ya wachezaji muhimu kikosini, Mpaka kumvutia kocha na uongozi wa klabu na kufikiria kumpa mkataba mpya mchezaji huyo.

Klabu ya Tottenham ina mipango ya muda mrefu ya kutengeneza timu ambayo itakua moja ya timu bora duniani, Hivo njia mojawapo ya kuhakikisha mipango yao inakamilika ni kuwapa mikataba mirefu wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa.

Acha ujumbe