Reguilon Arejea Spurs

Beki wa kushoto raia wa kimataifa wa Hispania Sergio Reguilon amerejea ndani ya klabu yake ya Tottenham Hotspurs akitokea klabu ya Manchester United ambapo alienda kwa mkopo katika dirisha kubwa lililopita.

Beki Reguilon amerejea ndani ya timu hiyo baada ya kutumikia mkataba wake wa mkopo wa miezi sita ndani ya klabu ya Manchester United, Hivo imeelezwa amesharejea kwenye kambi ya klabu yake ya Tottenham.reguilonMkataba wa mkopo wa beki huyo ndani ya Man United ulikua una uwezekano wa kua msimu mzima, Lakini Manchester United wamesitisha mkopo huo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa zinaeleza beki huyo hakua na furaha ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Hivo kufikia mamuzi ya kukubaliana na klabu hiyo kusitisha mkataba wake ndani ya klabu hiyo.reguilonBeki Reguilon sasa amerejea kwenye klabu yake ya Tottenham Hotspurs ambapo anapaswa kwenda kupambania nafasi pia, Kwani mchezaji huyo amekua akikosa nafasi klabuni hapo na akitolewa kwa mkopo vilabu tofauti tofauti.

Acha ujumbe