Klabu ya Tottenham Hotspurs inaelezwa itaingia sokoni mwezi Januari mwakani kwajili ya kutafuta beki wa katikati ambaye atakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo.
Kocha Ange Postecoglou leo akiongea na waandishi wa habari ameweka wazi kua klabu hiyo itaingia sokoni mwezi Januari na nafasi ambayo watakwenda kuitolea macho zaidi ni ya beki wa katikati.Tottenham ina mabeki kadhaa wa katikati wenye uwezo lakini watahitaji kuongeza beki mwingine kwajili ya kuja kuimarisha na kukipa nguvu kikosi hicho kuelekea ungwe ya pili ya msimu.
Beki Matty Van di Vien mpaka sasa anaandamwa na majeraha beki huyo ambaye amjiunga na klabu hiyo katika dirisha kubwa lililopita, Hivo watahitaji beki mwingine kutokana na majeraha pia ambayo yamekua yakiandama wachezaji wa klabu hiyo.Kocha Ange wa Tottenham anasema watahitaji kuongeza beki mwingine wa katikati kwani hawaezi kujua nini kinaweza kutokea siku za usoni, Hii inaonesha kuna mambo yanayoweza kutokea kama majeraha, kadi nyekundu ambayo yanaweza kuwakwamisha katika michezo mingine kama watakua hawana mchezaji mwingine mwenye ubora.