Neymar na Wachezaji wa Brazil Watuma Ujumbe Maalum kwa Pele Akiwa Hospitali

Neymar na Richarlison waliongoza sherehe za kumuenzi Pele huku wakituma ujumbe wa kumuunga mkono shujaa wa taifa la Brazil na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia ambaye kwa sasa anapambana na Uviko-19 na saratani ya utumbo mpana.

 

pele

Nyota wa Brazil wametuma ujumbe wa kumuunga mkono gwiji wa soka wa taifa lao Pele baada ya kuifunga Korea Kusini katika mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia siku ya Jumatatu huku Mbrazil huyo akimtazama akiwa hospitalini.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 82 anayechukuliwa na wengi kama mwanasoka bora zaidi wa wakati wote kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kwa ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na Uviko-19 kulingana na taarifa.

 

pele

Pele pia anapokea matibabu ya saratani ya utumbo ” chemotherapy”, huku Brazil ikijitahidi kutwaa taji la sita kombe la dunia.

Wachezaji wa Brazil walikuwa na nia ya kuonyesha uungwaji mkono wao kwa nyota huyo wa taifa baada ya kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia kwa ushindi mnono dhidi ya Korea Kusini.

Neymar aliyerejea akiwa majeruhi, winga wa Real Madrid Vinicius Jr, nyota wa Tottenham Richarlison, na kiungo Lucas Paqueta walifunga mabao nchini Qatar huku ndoto za Korea Kusini za Kombe la Dunia zikihitimishwa kwenye hatua ya 16 bora. Beti hapa mechi za kombe la dunia zilizobaki.

 

pele

Wafungaji mabao Richarlison na Neymar walikuwa na nia ya kuwahusisha wenzao walipoanza kufunua bendera ya kumuenzi Pele uwanjani kwa muda wote katika Uwanja wa 974 ambao jana ulikuwa ni siku ya mwisho kwa uwanja huo kutumika.

Wachezaji wa Brazil walijumuika na wafanyakazi wa timu hiyo kupiga picha na bango kubwa lenye picha ya Pele ambalo lilitaja tu jina lake ambayo alikuwa akisherehekea mafanikio ya Kombe la Dunia na taifa hilo wakati wa enzi zake za kucheza.

Pele alishinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa na Brazil mwaka 1958, 1962 na 1970, na alifunga mabao 643 katika mechi 659 rasmi za klabu ya Santos ya Brazil. Alifunga mara 77 katika michezo 92 ya timu ya taifa ya nchi yake.

Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.