United Kimewaka Tena

Klabu ya Manchester United ambayo inachechemea kunako ligi kuu nchini Uingereza baada ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo ya ligi hiyo,Inadaiwa kumekua na hali ya kutokuelewana katika vya kubadilishia nguo vya klabu hiyo.

Watu wa ndani wa klabu hiyo wameeleza kuna hali ya wachezaji wa United kutokufurahishwa na mbinu za mwalimu wao mdachi Eric Ten Hag ambae ndo kwanza amefika majira haya ya joto kunako klabu hiyo yenye maskani yake jijini Manchester.

Man United Dress Ten Hag

Hali hii imekua kama ya mazoea katika klabu hiyo ambapo kumekua na mfululizo wa wachezaji kupishana na walimu wanaofundisha Man United.

Ikumbukwe kulikua na hali ya kutokuelewana ya mwalimu Jose Mourinho baina yake na baadhi ya wachezaji nyota wa klabu hiyo,Halikadhalika aliewahi kua nyota wa klabu hiyo ambae alifundisha pia na kutimuliwa  Ole Gunnar Solskjaer.

Sababu tofauti tofauti zimekua zikitajwa juu ya kutokuelewana huko ila kwasasa sababu kubwa inayotajwa ni mbinu za mwalimu huyo mdachi kushindwa kueleweka na wachezaji wake.

Pia nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire kuendelea kuwa nahodha na kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Wakati ikidaiwa kuwa wachezaji wengi hawafurahishwi na hali hiyo.

Wachezaji hao wanaamini nahodha wao huyo hastahili kuwa kiongozi wa klabu hiyo, wala kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji uwezo wa chini dimbani na wanapigharimu klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.