Zikiwa ni siku si nyingi baada ya mchezaji aliyekuwa akikipiga katika ligi kuu ya Uingereza na kwenye klabu ya Liverpool Sadio Mane kuondoka na kwenda kwa wababe wa ligi kuu ya Ujerumani Bayern (Bundesliga) ameendelea kufanya vizuri zaidi.

Sadio Mane ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Senegal na mshindi wa kombe la Afcon ameendelea kuuthibitishia Ulimwengu kuwa bado ana ubora wake kwenye mpira ambapo anaendelea kufunga mabao kwenye timu yake mpya ambayo ni Bayern Munchen aliyosajiliwa msimu huu wa 2022/2023.
Mpaka sasa kwenye mechi sita za Bayern ambazo amecheza amefunga mabao matano kitendo ambacho kinamfanya ajione ni bora na azidi kujiamini, Bayern ambayo ina wachezaji wenye viwango vikubwa inahitajika nguvu ya ziada na kujituma ili uweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa kumshawishi mwalimu.

Bayern baada ya kumuuza mfungaji wake wa muda wote Roberto Lewandowski walikuwa wanahitaji mtu kama Sadio kwaajili ya kufunga mabao mengi kwani Bayern inashiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya ambayo inatarajiwa kuanza siku chache zijazo na mabao mengi ndiyo yatakufanya usonge mbele.
Katika mechi nne ambazo amecheza ameshinda tatu na sare moja huku akiwa hajapoteza mchezo wowote na alama zake kumi akiwa sawa na Union Berlin ambaye hupo nafasi ya pili ya msimamo.

