Mabao mawili ya Rafael Leao yaliwatia moyo AC Milan kupata ushindi mnono wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao Inter Milan katika mchezo wa kusisimua uliomalizika kwa jumla ya mabao matano katika siku ya Dabi ya Milan, Jumamosi.

Inter walichukua uongozi wa mapema uliowekwa kimiani na Marcelo Brozovic, lakini AC walibadilisha mchezo kwa mabao ya Olivier Giroud na bao la kujifunga la Leao. Edin Dzeko aliingia akitokea benchi na kupachika nyavu mara moja na kupunguzamachungu kwa Inter, lakini AC Milan walisimama kidete kulinda uongozi wao na kutwaa pointi zote tatu.

AC walikamilisha mechi hiyo dakika ya 53 wakati Giroud, ambaye alionekana kutisha muda wote, aliondosha mpira hadi nje ya eneo la hatari. Leao alifunga bao lake la pili la mechi muda mfupi tu baada ya kufanya mkimbio wa hatari zaidi ambao ulimfanya aipatie timu yake goli.

Leao kijana mwenye umri wa miaka 23, mshambuliaji wa kimataifa wa ureno jana alionesha soka la kiwango kikubwa sana kwa kufunga goli mbili na ndiye aliyechaguliwa mchezaji bora wa mechi “man of the match“

Timu zote zitahitaji kutimua vumbi na kujiandaa kuanza mechi zao za Ligi ya Mabingwa (UCL) wiki hii. AC Milan, walio kundi moja na Chelsea, watasafiri kuwakabili FC Red Bull Salzburg Jumanne jioni, huku Inter Milan wakiwakaribisha Bayern Munich Jumatano usiku.

