Thomas Tuchel anaweza kufanya chaguzi la kumtoa golikipa wake namba moja Edouard Mendy katika kikosi kitakachoanza leo hii kwenye mechi ya kwanza ya ligi ya mabingwa ambapo Chelsea watakuwa wageni wa Dinamo Zagreb.

Huku akifanya mchanganyiko wa wachezaji katika kikosi chake kabla ya ujio wa kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza mwezi November. Na Mendy akiwa ni mchezaji mojawapo ambaye hajafurahishwa na mwanzo mzuri wa msimu huu licha ya kuoka mipira kadhaa.
Golikipa aliizawadia Leeds united bao wakati The Blues wakilala kwa mabao 3-0 katika uwanja wa Leeds Elland Road ambapo bao hilo lilifungwa karibu na lango lake kwa makosa yake binafsi. Golikipa huyo amekuwa na makosa yakujirudia ya namna hiyo kitendo ambacho kinafanya mashabiki wa timu hiyo kukasirishwa sana pamoja na Tuchel.

Baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa leo hii vijana wa Tuchel mchezo wa wikiendi wakuwa wakikipiga dhidi ya Fulham ambao timu hiyo ikiwa ni bora kati ya timu zile zilizopanda daraja huku ikiwa na washambuliaji hatari ambaye ni Aleksandar Mitrovick aliyetupia mabao mechi nne mfululizo vilevile wamemuongeza Willian aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea.
Mechi hiyo itakuwa ni mechi ya kumuungalia Mendy kama ataweza kuwa namba moja au ampishe kidogo Kepa Arrizibalaga ambaye bado ni kipa ghali zaidi na amekuwa hapewi nafasi sana katika kikosi hicho lakini ameamua kusalia klabuni hapo msimu huu.

Mendy ambae ni golikipa namba moja wa Taifa la Senegal na Chelsea mpaka sasa ameruhusu mabao tisa katika mechi tano zilizopita, huku rekodi hiyo ya hivi karibuni ikimtofautisha na kiwango chake cha awali alichokuwa nacho.

