Rafael Nadal gwiji wa mchezo wa tenesi duniani na mwanatenesi anayeongoza kwa mataji makubwa ya tenesi maarufu kama Grand Slams amekubali kua alizidiwa kwenye michuano ya wazi ya Marekani.
Gwiji huyu mzaliwa wa jijib la Madrid nchini Hispania alipoteza pambano hilo kwenye raundi ya nne dhidi ya Frances Tiafoe ambaye alimmudu gwiji huyo na kumaliza mchezo raundi ya nne tu na Nadal kukiri alikua bora kuliko yeye.
Nadal amekiri kutokucheza vizuri mchezo huo na alihitajika kucheza vizuri zaidi ya alivyocheza wakati huo akitoa sifa kwa mpinzani wake huyo kua alistahili kushinda kwakua alicheza vizuri kuliko yeye.
Rafael anaendelea kushikilia rekodi ya mwanaume ya mwanaume mwenye mataji mengi makubwa akiwa na jumla ya mataji 22 mbele ya manguli kama Novak Djokovic mwenye 21 akifuatiwa na Roger Federer mwenye mataji 20.

