Kocha mkuu wa klabu ya Barcelona Xhavi Hernandez amesema kuwa kuwa na ndoto ni bure, kwanini tusishinde? . Xhavi amesema kuwa Barcelona wanaweza kuwa wafalme wa ligi ya mabingwa tena.

 

Xhavi: "Kuwa na Ndoto ni Bure,"

 

Xhavi anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kunyanyua ndoo ya mabingwa tena baada ya kukaa takaribani muda wa miaka saba bila kuchukua ubingwa huo huku mara ya mwisho kubeba ubingwa huo ikiwa ni 2015.

Kocha huyo amekituma kikosi chake hicho kwenda kufanya vizuri kwenye mechi yao ya kwanza ya ufunguzi ambapo watacheza dhidi ya Viktoria Plizen siku ya Jumatano, huku akitamani waepuke kurudiwa kwa mchujo wa mwisho wa hatua ya makundi ya kampeni.

Xhavi: "Kuwa na Ndoto ni Bure,"

Barcelona walimaliza nyuma ya Bayern na Benfica huku Xhavi akiteuliwa kuwa kocha katika klabu hiyo baada ya Ronald Koeman kutimuliwa. Barca walipoteza kwa kipigo cha mabao 3-0 na kusababisha Xhavi kushindwa kuendelea mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwenye raundi ya mtoano.

Hatahivyo timu hiyo imefanya usajili wa wachezaji wakubwa wenye ubora akiwemo Robert Lewandowski, ambao wanaibeba timu hiyo na kufanya timu hiyo kuwa katika sura mpya na kuwa ni timu yenye ushindani.

Kufeli kwa Barcelona msimu uliopita kuliumiza sana huku wapinzani wao wakubwa Real Madrid wakibeba ubingwa huo kwa mara ya 13. Kocha wa Barca amesema kuwa,

Xhavi: "Kuwa na Ndoto ni Bure,"

 

“Lengo kuu kwa sasa ni kupita hatua ya makundi” Kuota ni bure kwanini tusishinde mashindano haya?. Lakini inabidi tuanze kwa kuchukua alama tatu hapo kesho”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa