Marcelo Viera da Silva Junior ndo pasipoti yake inavyosoma gwiji na nahodha za zamani wa klabu ya Real Madrid ametambulishwa rasmi ndani ya klabu ya Olympiacos ya nchini ya Ugiriki.
Beki huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil ambae aliitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ametambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki wa klabu ya Olympiacos akiwa na familia yake.
Marcelo amekubali kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia klabu hiyo kongwe na yenye mafanikio nchini Ugiriki.
Nyota huyo alieitumikia klabu ya Real Madrid kwa miaka kumi na tano ni rasmi amejiunga na Olympiacos na atavaa jezi namba 12 kama ambayo alikua akiivaa ndani ya klabu ya Real Madrid kwa niaka yote akiyohudumu klabuni hapo.

