Rais Juventus asisitiza Allegri Bado Yupo Sana.

Rais wa klabu ya Juventus Andrea Agnelli amesisistiza kocha wa klabu hiyo Massimiliano Allegri ataendelea kusalia klabuni hapo licha ya matokeo mabaya anayoendelea kuyapata.raisRais wa klabu hiyo ameyaeleza hayo jana baada ya klabu hiyo kupoteza mchezo dhidi ya klabu ya Maccabi Haifa ya nchini Israel kwa mabao mawili kwa bila na kuendeleza matokeo mabovu ndani ya timu hiyo.

Licha ya matokeo hayo mabaya ambayo klabu hiyo inayapata katika ligi ya mabingwa ulaya na ligi ya nyumbani lakini Agnelli amesisitiza bado waa imani na kocha Allegri klabuni hapo.

“Allegri ni kocha wa Juventus. Na atabaki hivo” Hata alipoulizwa Rais huyo kama wanaogopa kumfukuza kocha huyo kwasababu ya kuhofia kumlipa fedha nyingi Agnelli alikanusha suala hilo.raisKlabu ya Juventus imepoteza ubora wake ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo wakiwa chini ya kocha Allegri na jambo hilo linawakera mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaamini timu yao inapaswa kufanya vizuri kwasababu wanaamini timu yao ni wafalme haswa baada ya kubeba ubingwa wa Serie A kwa takribani misimu nane mfululizo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.