Varane Kurejea Hivi Karibuni

Beki wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane ana uwezekano mkubwa wa kurejea hivi karibuni baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita.

Beki huyo ambae hatarajiwi kucheza mchezo wowote wa klabu mpaka michuano ya kombe la dunia litakapoanza mwezi Novemba mwaka huu. Hii ilikua katika mchezo dhidi ya klabu ya Chelsea ambapo Vrane alipata maumvivu ya mguu wake na kushindwa kuendelea na mchezo huo.varaneMatumaini ya mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa yaliibuka baada ya beki huyo kuposti kwenye mtandao wake wa kijamii na akionekana akifanya mazoezi kwenye makao makuu ya kambi ya timu ya taifa ya Ufaransa na kuandika “Asanteni kwa jumbe zenu za pole, Nimekua nikifanya mazoezi na naendelea vizuri”

Huku maelezo ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps kua ataenda Qatar kwenye michuano ya kombe la dunia na wachezaji waliofiti tu, Sasa maswali yakiwa mengi je beki huyo atakua fiti mpaka michuano ya kombe la dunia itakapoanza.varaneBeki Varane pia ameacha pengo kwenye klabu yake ya Manchester United baada ya kupata majeruhi kwani alitengeneza ukuta mgumu na beki mwenzake kwenye timu hiyo Lisandro Martinez.

Faida kwa klabu ya Man United ni beki huyo anakosekana na ligi zinasimama ili kupisha michuano ya kombe la dunia ambayo yanaanza hivi karibuni nchini Qatar, Huku zikiwa zimebakia Takribani wiki tatu tu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.