Mshambualiaji wa zamani wa klabu ya Simba Meddie Kagere amefunguka chanzo cha yeye kuondoka klabuni hapo na kuweka wazi kocha aliepita klabuni hapo hakumtaka.
Mshambuliaji huyo aliyejijengea umaarufu nchini Tanzania na kua kipenzi cha mashabiki wa Simba kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao, ameeleza kua kocha aliepita klabuni hapo Zoran Maki hakua akimuhitaji ndo maana yeye alilazimika kuondoka ndani ya klabu ya Simba.
Mshambuliaji huyo wa sasa wa Singida Big Stars ameeleza kua kocha huyo alipokuja klabuni hapo alihitaji washambuliaji wapya wawili wakati huo tayari kuna washambuliaji wawili yaani Kagere na Mugalu. Hivo mshambuliaji huyo anaeleza akajiongeza tu kua anachotakiwa kufanya ni kutafuta timu nyingine.
Kagere anaeleza kua viongozi wa klabu hawakutaka aondoke lakini kwakua kocha ametaka aondoke na klabu inamtaka kocha hawakua na namna nyingine. Pamoja na hivo klabu ilitaka imtoe kwa mkopo lakini mshambuliaji huyo akaona kuliko aondoke kwa mkopo bora auzwe.
Kocha aliepita klabuni hapo Zoran Maki raia wa Serbia ndio alionesha kutomhitaji mshambuliaji huyo, Na kuhitaji washambuliaji wengine na kumuona mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Rwanda hafai kwenye mfumo.

