Chelsea Yapata Pigo Jingine Tena

Klabu ya Chelsea imepata pigo jingine hapo jana baada ya beki wao mwingine Ben Chilwell kuumia kwenye mchezo wa jana wa klabu bingwa Ulaya walipokuwa wakicheza dhidi ya Dinamo Zagreb.

 

Chelsea Yapata Pigo Jingine Tena

Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kushinda kwa mabao 2-1, huku kocha wa timu hiyo Graham Potter akihofia kuwa huenda mchezaji huyo asipone kwa haraka baada ya ktoka uwanjani akichechemea, huku zikiwa zimesalia siku 19 tu kabla ya Uingereza kuanza kampeni yao ya kombe la Dunia.

Kwahiyo mpaka sasa Potter ana wachezaji wawili ambao ni majeruhi katika eneo hilo la beki wa pembeni wakwanza akiwa ni Recce James aliyeumia kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Milan na sasa Ben Chilwell nae ameumia.

Chelsea walitanguliwa kufungwa bao mapema kabisa katika dakika ya 7 ya mchezo na baadae Sterling akaja kusawazisha bao hilo, lakini ndani ya dakika 45 za kwanza The Blues walipata bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Denis Zakaria huku ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza kucheza toka atue Darajani.

Chelsea Yapata Pigo Jingine Tena

Potter amekiri kuwa  jeraha la beki huyo wa kushoto linaonekana “sio kubwa” na kuwaacha Chelsea na England wakiwa na wasiwasi juu ya utimamu wa beki huyo wa kushoto huku akisema kuwa hana matumaini kwa sasa kuhusu jeraha la Chilwell na ni pigo kwao baada ya mchezo mzuri .

Potter amekuwa kocha wa kwanza wa Chelsea tangu Roberto Di Matteo, ambaye alishinda shindano hilo msimu wa 2011-12, kutopoteza katika mechi zake tano za kwanza za Ligi ya Mabingwa akiwa kocha.

The Blues tayari walikuwa wamefuzu kwa hatua ya mtoano wakiwa vinara wa Kundi E, baada ya kushinda mechi zao nne, sare moja na kipigo mara moja, huku Graham akiiambia BT Sport kuwa;

Chelsea Yapata Pigo Jingine Tena

“Nimefurahishwa sana kupata ushindi huo. Nilidhani Denis alikuwa mzuri sana, alicheza kwa ari alisonga mbele na nimefurahishwa naye. Ilikuwa mechi nzuri ya kwanza. Wasiwasi utakuwa kama hautengenezi nafasi, lakini nia yetu ilikuwa nzuri, uchezaji wetu ulikuwa mzuri na ubora ulikuwepo kutoka kwa wachezaji”.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.