Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Brazil Carlos Casemiro amesema anamtakia kila kheri aliekua mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo ambaye ametangaza kuondoka klabuni hapo siku za hivi karibuni.
Kiungo huyo amesema anasikitishwa na kuondoka kwa nyota huyo kwakua walikua marafiki na kusema yeye anamtakia kila kheri kila kheri katika safari yake inayofata lakini akisisitiza isipokua watakapokua wamekutana katika timu tofauti.
Ronaldo na Casemiro wamefanikiwa kucheza timu mbili tofauti kwa wakati mmoja kwani wachezaji hao walicheza katika klabu ya Real Madrid kwa miaka mitano yenye mafanikio na wakati huu wakakutana tena katika klabu ya Manchester United kabla ya Ronaldo kuondoka.
Cristiano Ronaldo ametangaza kuondoka katika klabu ya Manchester United baada ya kukubaliana na klabu hiyo kuvunja mkataba uliokua umebakia na sasa nyota huyo atakwenda timu nyingine punde tu baada ya micguano ya kombe la dunia kumalizika.
Casemiro ameyazungumza hayo katika mkutano na waandishi wa habari wakati wakijiandaa kucheza mchezo wao wa pili wa kundi kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi ya Uswisi hapo kesho.

