Gwiji wa zamani wa klabu ya Juventus Allesandro Del Piero ameonekana yupo tayari kuisaidia klabu hiyo ambayo inatafuta mrithi wa aliekua rais wa klabu hiyo Andrea Agnelli ambaye amejiuzulu nafasi yake klabuni hapo pamoja na wasaidizi wake.
Siku ya jumatatu baada ya klabu hiyo kufanya mkutano wa bodi ilitangaza aliekua rais wa klabu hiyo Andrea Agnelli, makamu wake wa rais Pavel Nedved pamoja na mkurugenzi mkuu Maurizio Arrivabene wakitangaza kujiuzulu nafasi ambazo walikua wamezishikilia.
Exor ambao wanaongoza kwakua na hisa klabuni hapo walionesha kua Gianluca Ferrero anaweza kuchukua nafasi ya Andrea Agnelli klabuni hapo, Lakini maamuzi ya kutambua nani atachukua nafasi hiyo yatafanyika Januari 18 utakapofanyika mkutano wanahisa wa klabu hiyo.
Del Piero akiongea na waandishi wa habari na kuulizwa kama ataweza kuchukua nafasi ya uongozi wa klabu hiyo yeye akisema yupo tayari kuisaidia klabu hiyo kwakua ni mtu aliedumu klabuni hapo kwa takribani miaka 20 hivo suala la kuisaidia timu hiyo sio la kuuliza.
Kiungo huyo fundi wa zamani wa kibibi kizee cha Turin alikazia kua aliwahi kushuka daraja na timu hiyo na kuipandisha tena na hiyo ilitokana na mapenzi yake na Juventus,Huku akieleza ana uhusiano mzuri na timu hiyo kuanzia uongozi mpaka mashabiki wa timu hiyo.
Del Piero anaeleza kua hajapata simu yeyote kutoka Juventus kumtaka akachukue nafasi klabuni hapo lakini kwa upande wake ikitokea atakua tayari kwani yuko tayari kuipambania timu hiyo kama alivyokua mchezaji.

