Azam waweka mikakati ya ubingwa

Uongozi wa klabu ya Azam FC umeweka wazi kuwa tayari umeweka mipango ya kuhakikisha wanachukua ubingwa wa ligi kuu Bara kwa msimu huu.

Azam waweka mikakati ya ubingwa

Kikosi cha Azam kwa sasa kinaendelea kujifua kwa ajili ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Desemba 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Akizungumzia maandalizi yao, Kaimu Ofisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe alisema “Kikosi chetu kipo vizuri na kinaendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania.

“Timu itaondoka kwa njia ya ndege kesho jumamosi kuelekea Moshi tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Azam waweka mikakati ya ubingwa

“Akaminko alipata changamoto kidogo mazoezini lakini kwa sasa yupo vizuri na mashabiki wategemee kumuona kwenye huo mchezo.

“Tunahitaji ubingwa hivyo tumeweka mikakati ya kushinda katika michezo 10 mfululizo na baada ya hapo itakuwa michezo 15 tukifanikiwa tutakuwa tumetwaa ubingwa wa ligi kuu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.