Wenger: Siasa Zimewaponza Ujerumani

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema chanzo cha timu ya taifa ya Ujerumani kutolewa mapema kwenye michuano ya kombe la dunia inachangiwa na timu hiyo kujiingiza kwenye maandamano ya kisiasa.

Ujerumani wametolewa kwenye michuano ya kombe ya kombe la dunia kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi na kukusanya jumla ya alama nne sawa na Hispania lakini wakizidiwa kwa idaidi ya magoli.wengerMechi ya kwanza ambayo Ujerumani walipoteza walipiga picha ya kufunika mdomo kuonesha ishara ya kupinga maamuzi ya nahodha wao Manuel Neurer kuzuiwa kuvaa kitambaa cha unahodha chenye alama ya One Love ikimaanisha kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja wakati Qatar imezuiliwa.

Timu hiyo ilionesha imejiingiza kwenye maandamano ya kisiasa jambo ambalo kocha wa zamani wa Arsenal ambaye kwasasa ni mkuu wa kitengo cha utafiti Fifa alizungumza “Timu ambazo zina uzoefu wa kucheza mechi za kombe la duni kama Ufaransa na Uingereza zilishinda mechi zao za kwanza. Na timu hizo ni timu ambazo zilikua tayari kiakili na sio maandamano ya kisiasa”wengerMbali na kocha huyo wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger pia mchezaji wa klabu ya Real Madrid alizungumza siku kadhaa nyuma kua wachezaji wa Ujerumani wamevurugwa kiakili baada ya kujiingiza kwenye kampeni za kisiasa ambazo hawakutakiwa kujiingiza kama wachezaji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.