Klabu ya Tottenham Hot Spurs inayoongozwa na kocha mkuu Antonio Conte wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Marekani na Juventus Weston McKennie.

McKennie ambaye ana umri wa miaka 24, alikuwa sehemu muhimu ya safu ya kati ya nchi yake wakati wa kampeni yao ya Kombe la Dunia walipotolewa na Uholanzi katika hatua ya 16 bora.
Mchezaji huyo wa Juventus alianza michezo yote minne na kutekeleza jukumu la No8 kwa ukamilifu katika timu yake na kufanya Spurs kuvutiwa naye katika majira ya joto ya dirisha la usajili Januari.
Kulingana na Calciomercato wanasema kuwa mchezaji huyo mzaliwa wa Texas anaweza kwenda Spurs Januari.

Mashindano ya kuwania nafasi mjini Turin yamemaanisha kuwa McKennie amecheza dakika 90 mara tatu pekee kwenye Serie A msimu huu huku akipigania nafasi chini ya Max Allegri.
Akiwa na mchango wa mabao manne katika michuano yote, mchezaji huyo wa Kimataifa wa Marekani mwenye mechi 40 atatoa nafasi ya ziada katika safu ya kiungo ili kuwapa changamoto wachezaji kama Rodrigo Bentancur na Pierre-Emile Hojbjerg.
Ripoti zinaonyesha kuwa dili litakuwa gumu kufikiwa kutokana na uhusiano kati ya Bibi Kizee na Fabio Paratici huku klabu hiyo ikiendelea kuchunguzwa kwa makosa ya kifedha.

Hata hivyo, mapambano ya wababe hao wa Italia yanaweza kuleta mafanikio kwa klabu hiyo ya Kaskazini mwa London, kukiwa na uwezekano wa kuwa na mikataba nafuu ya kusawazisha hapo Turin.

