Liverpool waliondoka kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu Jumatatu alasiri, ambapo wataanza maandalizi ya nusu ya pili ya msimu.

Sehemu ya wachezaji waliosafiri ni pamoja na Luis Diaz, Diogo Jota, Naby Keita na Arthur Melo, ambao wataendelea kufanyia kazi programu zao za mazoezi baada ya kutoka kwenye majeraha yao.
Liverpool itamenyana na Olympique Lyonnais na AC Milan katika mechi mbili za Dubai Super Cup, na zote zitakuwa Meridianbet na odds zake kubwa beti hapa, kabla ya kurejea Merseyside kabla ya mechi ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City mnamo Desemba 22.

Wachezaji wanaoshiriki Kombe la Dunia kwa sasa watajiunga tena na kikosi katika tarehe za baadaye, huku Darwin Nunez akitarajiwa kuwasili wiki ijayo.
Kikosi cha Liverpool kilichoweka kambi ya mazoezi ya Dubai ni kama ifuatavyo:
Adrian, Kelleher, Davies, Mrozek, Pitaluga, Salah, Milner, Oxlade-Chamberlain, Jones, Elliott, Tsimikas, Ramsay, Robertson, Carvalho, Bajcetic, Phillips, Gordon, Keita, Matip, Gomez, Jota, Arthur, Diaz, Thiago, Firmino, Chambers, Quansah, Clark, Frauendorf, Stewart, Doak, Cain, Corness.


