Van Dijk: "Liverpool Itastawi Bila Kujali Ataimiliki Nani"

Beki wa kati wa Liverpool Virgil van Dijk ana imani thabiti kuwa timu yao itasalia kuwa na nguvu katika soka la Dunia bila kujali nani anamiliki ataimiliki timu hiyo iliyopo chini ya kocha mkuu Jurgen Klopp.

 

Van Dijk: "Liverpool Itastawi Bila Kujali Ataimiliki Nani"

 

Ilithibitishwa mwezi uliopita kuwa Klabu ya Fenway Sports Group (FSG) inachunguza uwezekano wa kuuza au kutafuta uwekezaji wa nje kwani wanalenga kuendelea na matumizi makubwa ya Ligi Kuu.

Ripoti zinaonyesha kuwa Liverpool wana thamani ya pauni bilioni 3.7 huku Morgan Stanley na Goldman Sachs wakisemekana kusimamia mchakato huo.

Van Dijk, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuisaidia Uholanzi kuishinda Marekani kwa mabao 3-1 na kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia, anasema Liverpool itaendelea kuimarika kwa yeyote atakayeiongoza Anfield.

Van Dijk: "Liverpool Itastawi Bila Kujali Ataimiliki Nani"

“Nina imani kamili na Liverpool kwamba watakuwa sawa. Sisi ni klabu iliyoimarika sana, moja ya klabu kubwa Duniani na ambayo itakaa hivyo, atakayekuja kuziba nafasi hizo atafanya vizuri sana, nafahamu kila kinachoendelea.”

Liverpool ilipitia wakati mgumu kupata matokeo mazuri kwenye Ligi kabla ya Kombe la Dunia na kushika nafasi ya sita kwenye Primia Ligi akiwa pointi 15 nyuma ya vinara Arsenal na saba nyuma ya Spurs katika nafasi ya nne.

Van Dijk: "Liverpool Itastawi Bila Kujali Ataimiliki Nani"

Van Dijk na timu yake walishinda mechi tano kati ya sita za Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi lakini walimaliza wa pili nyuma ya Napoli kwa tofauti ya mabao na watakutana na Real Madrid katika hatua ya 16 bora katika marudio ya fainali ya msimu uliopita, ambayo walifungwa 1-0.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.