Ten Hag Agoma kumzungumzia Sancho

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amegoma kumzungumzia mchezaji wake nyota wa klabu hiyo Jadon Sancho alipoulizwa na waandishi wa habari.

Mchezaji Jadon Sancho mara ya mwisho kucheza mchezo ndani ya Man United ilikua mwezi wa kumi dhidi ya Chelsea ambapo mchezo huo ulimalizka kwa kwa sare ya goli moja kwa moja, Baada ya hapo mchezaji huyo hajacheza mchezo wowote na klabu hiyo.ten hagWinga huyo wa zamani wa Borussia Dortmund pia hakusafiri na timu kuelekea nchini Hispania kipindi cha mapumziko ya kombe la dunia, Ambapo timu hiyo ilielekea kwajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili ligi michuano mingine.

Katika mchezo wa kombe la Carabao uliopigwa jana usiku katika dimba la Old Trafford ambapo ilishuhudiwa Man United ikiifunga Burnley kwa jumla ya mabao mawili kwa bila, Huku Ten Hag akiulizwa kuhusu kurejea kwa Sancho na kujibu hajui ni lini mchezaji huyo atarejea.ten hagWakati huo kocha Erik Ten Hag ameweka wazi kua beki wa kulia klabuni hapo ambaye inaelezwa anaweza kuondoka anaweza kusalia klabuni hapo kwa muda ujao, Aaron Wan Bissaka amekua hapati nafasi klabuni hapo lakini kocha huyo amesema bado ataendelea kusalia kwenye viunga vya Old Trafford.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.