Trezeguet: Rabiot ni Muhimu kwa Juventus

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa David Trezeguet amesema kiungo wa klabu hiyo Mfaransa mwenzake Adrien Rabiot anaweza kua msaada kwa kalbu hiyo siku za usoni.

Kiungo Rabiot amekua akihusishwa mara kwa mara kuondoka ndani ya klabu hiyo tangu amejiunga klabuni hapo akitokea PSG ya nchini Ufaransa, Mara ya mwisho ni dirisha kubwa lililopita ambapo alihusishwa kujiunga na klabu ya Manchester United.trezeguetKiungo huyo ambaye amekua na ubora mkubwa sana kwenye michuano ya kombe la dunia iliyopita nchini Qatar, Kwani alifanikiwa kucheza kwa kiwango cha hali ya juu na kuisaidia timu ya taifa ya Ufaransa kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Gwiji David Trezeguet anasema kiungo huyo ni mchezaji wa kiwango cha dunia na anaweza kua mchezaji muhimu kwenye klabu ya Juventus, Huku akiwataka klabu hiyo kuangalia namna wanaweza kumbakiza mchezaji huyo kwani wao ndo wahusika wakuu.trezeguetMshambuliaji Trezeguet ambaye amewahi kukipiga ndani ya Juventus amesema kiungo huyo atakua msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo, Huku akishirikiana na wachezaji wengine wazuri kama Angel di Maria pamoja na Paul Pogba.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.