KMC Watuma Salamu kwa Simba

Mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya NBC umekuwa mzuri kwa klabu ya watoza ushuru wa Kinondoni, KMC ni baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo baada ya ule na Coastal Union hatimaye Maafande wa Polisi Tanzania wamepigishwa kwata kwenye dimba la Uhuru Jijini Dar Es Salaam.

KMC walitangulia kupata bao la kwanza dakika za mapema sana kipindi cha kwanza kupitia kwa Kiungo wao wa kati Awesu Awesu mnamo dakika ya 10 tu, ilitosha kabisa kuwalaza Polisi Tanzania kwa kipindi cha kwanza bila kuambulia chochote.kmcNi yule yule mwenye jezi nambari 17 aliyewalazimisha sare Simba SC kwenye mzunguko wa kwanza, George Makang’a ndiye aliwaandikia bao la pili KMC kwa kichwa bomba kabisa ambacho kiliingia langoni bila kupingwa na mchezaji yeyote wa Pilisi Tanzania, kwaninwakati huo Mlinda mlango alikuwa kishatoka golini kwake kwenda kuokoa hatari ambayo alipigwa chenga malidadi na kisha mpira ukapigwa krosi iliyokutana na kichwa cha Makang’a.

Makang’a alipoulizwa na Meridian Sports kuhusu ushindi huo ikiwemo na yeye kufunga bao muhimu kwa timu yake alibainisha haya, haswa kuelekea mechi yao inayofuata na Simba SC

“Kwa sasa sijisikii vizuri kuzungumza lakini nafikiri nitafunga kama nilivyofunga leo hapa”

KMC sasa wanafisha jumla ya alama…. Na kuwafanya kupanda kwenye msimamo wa Ligi mpaka nafasi ya 8 nyuma ya….. Wenye alama….kmcMechi yao inayofuata ni kati ya Sima SC itakayopigwa Disemba 26, 2022 kwenye dimba la CCM Kirumba, na matokeo ya mechi ya kwanza walipokutana walitoka sare ya 2-2

Kocha wa KMC Thiery Hitimana alisema kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu na wataenda kwa kuiheshimu Simba.

“Najua mechi itakuwa ni nguma sana, Lakini tutaenda kwa kuiheshimu Simba kwa sababu ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri, ila na sisi (KMC) tuna wachezaji wazuri wa kupambana na kupata matokeo

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.