Alieyekua mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum Abdallah maarufu kama Fei Toto ameaga rasmi ndani ya klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii na kuonesha moja kwa moja kua anaondoka klabuni hapo.
Kiungo huyo ambaye inasemekana anaelekea mtaa wa Chamazi kujiunga na klabu ya Azam Fc matajiri wa wa Dar-es-salam, Kiungo huyo ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram pamoja na Twitter na kuwaaga mashabiki, wanachama, viongozi na wachezaji wa klabu hiyo.
Kiungo Feisal Salum amesema atakumbuka nyakati zote nzuri klabuni hapo na atajitahidi kusahau yote mabaya kwa haraka sana, Bila kusita kuelezea namna imemuwia vigumu kuweza kuwaaga wapenzi, mashabiki, viongozi na wachezaji wenzake lakini hakuna namna imebidi awaage.
Mchezaji Feisal Salum ambaye ameitumikia klabu ya Yanga kwa misimu takribani minne na nusu ndani ya klabu hiyo, Huku akiitumikia klabu hiyo kwa kiwango kikubwa kwenye mazingira ya shida na raha amewaaga rasmi Wananchi.
Klabu ya Azam Fc sasa ni wazi imetimiza lengo lake ambalo ilikua ikiliweka wazi tangu mwanzoni mwa mwezi uliomalizika, Sasa Feisal Salum anakwenda kuwatumikia matajiri hao wa jiji la Da-es-salam taarifa zikieleza mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu.

