Ihefu Waicharaza Mtibwa Sugar

Klabu ya Soka ya Ihefu fc kutoka mkoani Mbeya imefanikiwa kuiadhibu klabu ya Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro katika mchezo wa ligi kuu ya NBC mchezo ulipigwa katika dimba la Highland Estate jijini Mbeya.

Katika mchezo huo ulioonekana kua na kasi kwa pande zote mbili huku Ihefu wakionekana kuitafuta Mtibwa Sugar zaidi kwa mashambulizi ya hapa na pale, Lakini mchezo huu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyofanikiwa kuonalango la mwenzake.ihefuKipindi cha pili kilianza kwa kasi huku vijana hao kutoka mkoani Morogoro wakionekana kua na usongo zaidi kwani dakika ya 52 Ismael Mhesa alianadikia Mtibbwa bao la kuongoza, Lakini vijana kutoka jijini Mbeya kupitia kwa Joseph Mahundi dakika ya 60 akaisawazishia Ihefu bao na mchezo kua moja kwa moja.

Klabu ya Ihefu ilionekana kuamka zaidi baada ya kupata bao la kusawazisha na kutafuta bao la pili mpaka dakika 74 Obrey Chirwa akaipatia bao la pili Ihefu Fc, Na kuipa uongozi klabu hiyo katika mchezo huo.ihefuKlabu ya Ihefu iliofanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Joseph Mahundi mnamo dakika ya 88 ya mchezo na kuhakikisha klabu hiyo inavuna alama tatu muhimu kwenye mchezo huo, Na kufanikiwa kufikisha alama 17 katika msimamo wa ligi hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.