Manchester City wanaripotiwa kuwa tayari kumtoa Jack Grealish kwa AC Milan ili kubadilishana na mshambuliaji Rafael Leao.

City ya Guardiola wanamtaka mchezaji huyo wa Ureno mwenye miaka 23, na wanapambana na Chelsea ili kuinasa saini yake huku Calciomercato wakisema kuwa wanaweza kutoa saini yao ya rekodi ili kumaliza mkataba huo.
Grealish mwenye miaka 27, aliwasili Etihad kwa Pauni Milioni 100 mnamo Agosti 2021 na alishinda Ligi ya Primia katika msimu wake wa kwanza lakini amekuwa na wakati mgumu kuonesha kiwango kizuri mara kwa mara.

Mchezaji huyo wa zamani wa Aston Villa alitoa pasi mbili za mabao huku mabingwa hao wakirejea Ligi Kuu kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Leeds jana usiku. Lakini idadi yake tangu ajiunge na City ni ya kufunga mabao manne pekee na kutoa pasi tano za mabao katika mechi 35 za ligi.
Ripoti hiyo inaonyesha Pep Guardiola yuko tayari kumruhusu mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza kuondoka ili kumleta Leao.

Winga huyo wa Rossoneri ni mmoja wapo wa vipaji vinavyohitajika sana Serie A baada ya kufunga mabao saba na kutoa pasi tisa za mabao katika mechi 20 msimu huu, pamoja na mabao mawili ya Ureno kwenye Kombe la Dunia.
Na nyota huyo wa zamani wa Sporting na Lille amekiri kuwa yuko tayari kuhamia Ligi ya Primia siku zijazo. Kuhusu ikiwa kuhamia ligi kuu ya Uingereza kunamvutia, alisema: “Ndio, katika siku zijazo.

“Lakini sasa, ninalenga Milan kwa 100%. Niko kwenye klabu kubwa na niko chini ya mkataba. Pia napenda jiji hilo.”

