Aliekua kocha wa klabu ya Vipers ya nchini Uganda Roberto Oliveira ana asilimia kubwa za kujiunga na klabu ya soka ya Simba baada ya kumalizana na waajiri wake Vipers.
Kocha huyo ambaye leo amefanikiwa kuaga rasmi kunako klabu ya Vipers ya nchini Uganda, Taarifa zinaeleza kocha huyo ana asilimia kubwa sana za kujiunga na wababe wa Msimbazi kutokana na maamuzi yake ya kuachana na mabingwa hao watetezi nchini Uganda.
Kocha Roberto Oliviera aanaondoka katika klabu hiyo akiwa tayari amefanikiwa kuwapa taji la ligi kuu ya Uganda msimu uliomalizika, Lakini kumbukumbu kubwa ni pale alipoiwezesha klabu hiyo kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa Tp Mazembe.
Taarifa zinaeleza kua miongoni mwa makocha waliotuma barua ya maombi ya kutaka kazi kwenye klabu ya Simba jina la raia huyo wa Brazil lilikuepo, Na viongozi wa klabu hiyo wamekaa na kuchuja na wameona Roberto Oliveira ndio anafaa kuinoa timu yao.
Kama mambo yatakwenda kama inavyoelezwa basi kocha huyo wa zamani wa Vipers atajiunga na klabu ya Simba siku za karibuni kwenye michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar, Huku kocha wasasa Juma Mgunda ikielezwa ataendelea kua ndani ya timu hiyo kama kocha msaidizi.

