Ten Hag: Tunataka Mshambuliaji sahihi atakayeendana na Bajeti Yetu

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua klabu hiyo itaingia sokoni Januari kutafuta mchezaji sahihi lakini ambaye ataendana na bajeti yao ya usajili.

Kocha huyo ameelza hayo hayo ambapo aliulizwa na waandishi wa habari juu ya usajili wa mshambuliaji ndani ya timu ndipo aliposema wanahitaji mshambuliaji, Lakini lazima aendane na bajeti ambayo imewekwa na klabu hiyo lakini pia wanahitaji mtu sahihi.ten hagKufuatia kauli ya kocha huyo inaonesha ni wazi bajeti ya usajili ya klabu ya Manchester United kuelekea dirisha dogo la usajili Januari ni ndogo, Lakini pia ikumbukwe klabu hiyo ipo sokoni muda inatarjiwa kuuzwa hivo inawezekana inaweza kua sababu ya kutokupata fungu kubwa la pesa.

Klabu ya Manchester United inahitaji mshambuliaji ambaye ataweza kushirikiana na kwa ukaribu na Antony Martial pamoja na Rashford katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, Huku Martial muda mwingi akiandamwa na majeraha.ten hagKocha Erik Ten Hag pia amemzungumzia beki wake wa kulia Aaron Wan Bissaka ambaye ameonekana kucheza vizuri katika mechi mbili baada ya kombe la dunia, Kocha huyo akieleza kua mapumziko ya kombe la dunia yamemsaidia na amecheza vizuri kwenye mechi mbili na ndio kitu anachokihitaji kocha huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.