Wenger Matumaini Kibao Arsenal Kubeba Ubingwa Epl

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema anaiona timu hiyo ikiwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji la ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Klabu ya Arsenal jana imefanikiwa kushinda dhidi ya klabu ya Brighton kw mabao manne kwa mawili na kufanikiwa kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Arsenal wamefanikiwa kutengeneza pengo la alama saba dhidi ya klabu ya Man City ambao wanashikilia nafasi ya pili.wengerKocha Wenger anasema kwasasa klabu hiyo imekua imara zaidi na wana ubora mkubwa wa kuweza kugombania taji la ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Hiyo ni baada ya klabu hiyo kupata matokeo dhidi ya Brighton ndipo kocha huyo alipomwaga sifa kwa klabu yake hiyo ya zamani.

Kocha huyo anaamini Arsenal imeimarika sana kwasababu wana uwezo mkubwa sana wa kutengeneza nafasi katika kila mchezo, Na kocha huyo amesema yeye kiukweli haoni mapungufu kwenye kikosi hicho chini ya kocha Mikel Arteta.wengerWenger pia hakuacha kusifia uwezo wa nahodha wa timu hiyo Martin Odegaard ambaye amekua na kiwango bora sana kwa siku za hivi karibuni, Kocha huyo amesema mchezaji huyo anafanya ,pira kuonekana mrahisi sana na vilevile ameimarika sana na kupitia wachezaji kama yeye kwenye kikosi cha Arsenal anaamini wanaweza kutwaa ubingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.