Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag rasmi amechukua nafasi ya kuisimamia timu ya vijana chini ya miaka 21 ya klabu hiyo ili kuwezesha vijana wadogo wa timu hiyo wanaimarika na kuingia kwenye timu ya kwanza.
Kocha huyo ambaye amekua akisifika kwa uwezo wake wa kukuza vipaji vya vijana wadogo na kuwapa nafasi, Kocha huyo amefanya kazi hiyo kwa uweledi mkubwa akiwa katika klabu ya Ajax ambapo aliwapa nafasi vijana wadogo na kufanya vizuri kwenye timu ya wakubwa.
Kocha Ten Hag lengo kubwa la kuchukua jukumu la kuifundisha timu ya vijana ya klabu hiyo ni kuhakikisha anafatilia maendeleo ya vijana hao kwa karibu na kurahisisha vijana hao wenye vipaji vikubwa kwenye timu hiyo kupata nnafasi kwenye timu ya wakubwa ya Manchester United.
Kocha huyo ameona timu hiyo ya akiba imekua ikitengwa jambo ambalo ameona sio sahihi na kumfanya kuamua kuiongoza ili kuhakikisha timu hiyo inakua pamoja ili kuimarisha utamaduni wa klabu, Kocha huyo amewahi kufundisha timu ya akiba akiwa anaanza kazi ya ukocha kwenye klabu ya Bayern Munich.
Erik Ten Hag ambaye ana mipango mikubwa ndani ya timu hiyo na kufanikiwa kubadilisha mambo mengi ndani United tangu amejiunga hapo, Na hii inaonesha kwa namna gani kocha huyo ana uwezo wa juu katika mambo tofauti mbali na kufundisha ila pia ana uwezo wa kuweza kutengeneza umoja katika timu.

