Lukaku: Nataka Kusalia Inter Milan

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea aliopo kwa mkopo kwenye klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku ana mpango wa kusalia Inter Milan baada ya mkopo wake kumalizika.

Mshambuliaji huyo ambaye yupo kwa mkopo wa msimu mzima kwenye klabu ya Inter milan ya nchini Italia anasema anavutiwa kuendelea kusalia katika viunga vya San Siro, Hiyo ni kwasababu ana mapenzi makubwa na klabu hiyo.lukakuMshambuliaji huyo ambaye alipoondoka kwenye klabu ya Inter Milan aliwakera mashabiki wa klabu hiyo kwa kiasi kikubwa sana, Lakini yeye anasema mashabiki wa klabu hiyo ni mashabiki bora kuwahi kuwaona kwani hata kwenye kipindi kigumu wao wanatoa ushirikiano kwa timu yao.

Lukaku anaeleza kutokana na mapenzi yake na klabu ya Inter Milan anaeleza ana mpango wa kusalia klabuni hapo baada ya mkopo wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu, Na kusema atafanya mazungumzo na klabu ya Chelsea ili kupata suluhisho yeye aweze kusalia San Siro.lukakuMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku anasema alizungumza na wachezaji wenzake kwanini aliondoka na kwanini amerudi, Lakini kwasasa akili yake ipo ni kwa namna gani anaweza kuisaidia klabu ya Inter Milan kupataushindi kwasababu anasema klabu hiyo ni kila kitu kwake na ana mapenzi makubwa na Inter Milan.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.