Tottenham Yapasuka Nyumbani

Klabu ya Tottenham Hotspurs imepoteza mchezo wake wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa wakiwa katika dimba lao la nyumbani mapema leo.

Klabu hiyo ambayo ilikua inatafuta nafasi ya kukaa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini Aston Villa wamezima ndoto hiyo baada ya kuichabanga klabu hiyo mabao mawili kwa moja.tottenhamKatika mchezo huo ambao klabu ya Tottenham ilionekana kuukamata kwa kipindi kirefu lakini klabu ya Aston Villa wao walicheza kwa mahesbu makubwa na kuweza kupata alama tatu muhimu. Mabao ya Emiliano Buendia na Douglas Luiz yalitosha kuipa klabu ya Aston Villa alama tatu muhimu ugenini.

Vijana wa Antonio Conte wanashindwa kupata alama tatu katika mchezo wa pili mfululizo baada ya kushindwa kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Brentford wiki mwanzoni mwa wiki, Na leo wameshindwa tena kupata alama tatu dhidi ya Aston Villa.tottenhamBaada ya Tottenham kushindwa kuifunga Aston Villa sasa wanasalia katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza na alama zao 30, Huku wakishindwa kuishusha Manchester United wenye alama 32 wakiwa nafasi ya nne.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.