Tottenham Kuitafuta Nafasi ya Nne Leo Dhidi ya Villa

Klabu ya Tottenham leo itashuka dimbani kuzisaka alama ttu muhimu dhidi ya Aston Villa kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ili kurejea nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Vijana wa Antonio Conte leo watakua nyumbani dhidi ya vijana wa Unai Emery ambapo unatarajiwa kua mchezo wenye ushindani mkubwa, Kwani klabu ya Tottenham watakua wanatafuta alama tatu muhimu ili kurejea kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.tottenhamSpurs walidondosha alama mbili dhidi ya Brentford katika mchezo wa kwanza wa ligi hiyo baada ya kombe la dunia kumalizika baada ya kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Ni wazi kua klabu hiyo itakua ikihitaji alama tatu muhimu.

Klabu ya Aston Villa nao watakua na mikakati mikali kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu kwani wametoka kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya klabu ya Liverpool kwa mabao matatu kwa moja, Hivo mchezo wao dhidi ya Spurs ni muhimu kwao kwajili ya kujitengenezea mazingira mazuri kwenye ligi hiyo.tottenhamKlabu ya Tottenham kama watafanikiwa kupata matokeo ya ushindi leo dhidi ya Aston Villa watafanikiwa kufikisha jumla ya alama 33, Hivo watafanikiwa kuwashusha Man United waliopo nafasi ya nne na alama zao 32.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.