Aucho Bado yupo sana Jangwani

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kumuongozea mkataba kiungo wake makini kwenye dimba la kati Khalid Aucho raia wa kimataifa wa Uganda ambae ataendela kusalia kwenye klabu hiyo mpaka 2025.

Wananchi wamemuongezea mkataba kiungo huyo ambaye mkataba wake ulikua unamalizika ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Klabu ya Yanga imemuongezea kiungo huyo mkataba wa miaka miwili utakaomfanya awepo timu hiyo mpaka Juni 2025.auchoKhalid Aucho alijiunga na klabu ya Yanga mwaka 2021 na kusaini mkataba wa miaka miwili klabuni hapo mpaka mwaka 2023, Baada ya Yanga kuvutiwa na huduma ya kiungo huyo ndani ya klabu yao basi wameamua kumfunga pingu za kuendelea kusalia klabuni hapo.

Klabu ya Yanga ipo kwenye mchakato wa kuongezea mikataba wachezaji wake muhimu kwenye dirisha hili dogo mwezi Januari pamoja na kusaini nyota wengine. Kabla ya kumuongezea mkataba kiungo huyo walimuongezea mkataba golikipa wao namba moja klabuni hapo Djigui Diarra.auchoRais wa klabu hiyo Eng Hersi Camil yupo kwenye operesheni ya kuhakikisha wanawabakiza nyota wao muhimu kwenye klabuni hapo kwa kuwaongezea mikataba pamoja na kuiboresha, Wamefanikiwa kuanza na Djigui Diarra pamoja na Khalid Aucho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.