Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kumuongozea mkataba kiungo wake makini kwenye dimba la kati Khalid Aucho raia wa kimataifa wa Uganda ambae ataendela kusalia kwenye klabu hiyo mpaka 2025.
Wananchi wamemuongezea mkataba kiungo huyo ambaye mkataba wake ulikua unamalizika ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Klabu ya Yanga imemuongezea kiungo huyo mkataba wa miaka miwili utakaomfanya awepo timu hiyo mpaka Juni 2025.
Khalid Aucho alijiunga na klabu ya Yanga mwaka 2021 na kusaini mkataba wa miaka miwili klabuni hapo mpaka mwaka 2023, Baada ya Yanga kuvutiwa na huduma ya kiungo huyo ndani ya klabu yao basi wameamua kumfunga pingu za kuendelea kusalia klabuni hapo.
Klabu ya Yanga ipo kwenye mchakato wa kuongezea mikataba wachezaji wake muhimu kwenye dirisha hili dogo mwezi Januari pamoja na kusaini nyota wengine. Kabla ya kumuongezea mkataba kiungo huyo walimuongezea mkataba golikipa wao namba moja klabuni hapo Djigui Diarra.
Rais wa klabu hiyo Eng Hersi Camil yupo kwenye operesheni ya kuhakikisha wanawabakiza nyota wao muhimu kwenye klabuni hapo kwa kuwaongezea mikataba pamoja na kuiboresha, Wamefanikiwa kuanza na Djigui Diarra pamoja na Khalid Aucho.

