Kocha wa klabu ya Newcastle Eddie Howe amekanusha kua klabu hiyo ina mpango wa kumsajili nyota Cristiano Ronaldo katika dirisha kubwa la mwezi June.
Nyota Cristiano Ronaldo ambaye amejiunga na klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia ilielezwa hapo mwanzo kwenye mkataba wake na klabu hiyo kuna kipengele kitakachomruhusu kujiunga na klabu ya Newcastle kwenye majira ya joto mwezi wa sita, Ikiwa klabu hiyo itafuzu michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia ambayo imemsajili nyota Cristiano Ronaldo ina uhusiano na klabu ya Newcastle ya nchini Uingereza, Ikielezwa kua mmiliki wa klabu hizo mbili ni mmoja hivo ingeweza kurahisisha nyota huyo kujiunga na klabu hiyo.
Kocha Eddie Howe amesema hakuna kipengelea mabcho kinaonesha watamchukua nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kwenye dirisha kubwa la usajili na zaidi yeye anamtakia kila kheri nyota huyo katika klabu yake mpya ya Al Nassr huko nchini Saudia Arabia.
Klabu ya Newcastle chini ya kocha Eddie Howe mpaka sasa inaonekana kufanya vizuri huku ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 35, Hivo wanaonesha kila dalili ya kuhitaji kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya jambo ambalo wengi wanatafsiri inaweza kua njia ya Ronaldo kurudi tena ulaya jambo ambalo kocha wa klabu hiyo amelikanusha.

