Moukoko Akumbwa na Kashfa ya Kudanganya Umri

Kinda wa klabu ya ya Borussia Dortmund Youssoufa Moukoko mwenye umri wa miaka 18 amekutwa na kashfa ya kudanganya umri ikisemekeana umri wake halisi ni miaka 22.

Mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani amekumbwa na kashfa hiyo ikielezwa mchezaji huyo amedanganya umri kua ana miaka 18 lakini kumbe umri wake sahihi ni umri wa miaka 22.MoukokoMajarida mbalimbali duniani kama The sun na Daily Mail yameripoti kua cheti cha kuzaliwa cha Youssoufa Moukoko kinaeleza kua amezaliw mwaka 2000 na sio 2004 kama ambavyo yeye anaeleza na kumfanya aonekane ana miaka 18 badala ya 22.

Taarifa pia zinaeleza kua mchezaji Youssoufa Moukoko sio jina lake halisi na jina lake halisi kwenye vyeti vyake linasomeka kama Youssoufa Mohamadou, Hii inaendelea kumuweka kwenye matata kinda huyo wa kijerumani mwenye asili ya Cameron.MoukokoMpaka wakati huu mamlaka za soka nchini Ujerumani hazijatoa kauli yeyote kuhusu tuhuma hizo zinazomhusu mchezaji Moukoko, Huku wadau wengi wa soka wakisubiri majibu ya shirikisho la mpira wa miguu Ujerumani kwao wao ndio wanaweza kuuhakikishia umma ukweli wa mambo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.