Bruno Fernandes: Man United inacheza kitimu zaidi kwasasa

Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes amesema kua klabu hiyo imerudi kua kama timu baada ya ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya klabu ya Manchester City katika dimba la Old Trafford.

Kiungo Bruno Fernandes ambaye alifunga bao la kusawazisha baada ya mchezaji Jack Grealish kuwapa uongozi klabu ya Manchester City na baada ya kupata bao la ushindi kupitia kwa mshambuliaji Marcus Rashford, Na hiyo kuwafanya Manchester United kuwa nyuma kwa alama moja dhidi ya klabu ya Manchester City.Bruno fernandesKiungo huyo amzungumza wakati akifanya mahojiano baada ya mchezo na kusema “Nilisema kabla ya mchezo tunaonekana kama timu sasa, wakati fulani uliopita kila mmoja wetu alikua anajitafuta, Sasa unaona timu inayocheza kitimu na kila mmoja akicheza kwajili ya mwenzake”

Kiungo Bruno Fernandes ameweka bayana kua klabu hiyo chini ya kocha Erik Ten Hag kwasasa inaonekana kama timu inayoeleweka na inacheza kitimu, Hii akimaanisha klabu hiyo haikua inacheza kitimu siku za nyuma lakini kwasasa kutokana na ubora ambao wanaonesha kiwanjani na hali ya upambanaji inaonesha wanacheza kitimu zaidi.Bruno fernandesKiungo huyo pia alizungumzia suala la klabu hiyo kua nyuma kwa alama moja dhidi ya mahasimu wao klabu ya Manchester City na kueleza kua wao hawajali suala hilo zaidi wanaangalia zaidi mchezo unaofuata na wanahitaji kushinda, Lakini akiweka wazi kua endapo wao watafanya vibaya basi City wataenda mbali zaidi hivo wao wanapaswa kushinda michezo yao inayofuata na ikiwa ndio malengo yao makubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.